Wapendwa Marafiki Waislam,
1. Nina furaha ya pekee kuwapa matashi ya kirafiki
na upendo kutoka kwa Halmashauri ya Kipapa kwa ajili ya Mazungumzano na Dini
mbalimbali kwa nafasi ya furaha kwenu ya sikukuu ya ‘Id al-Fitri’,
inayohitimisha safari yenu mliyoifanya wakati wa mwezi wa Ramadhan wa mfungo na
sala.
Mchakato huu ni muda wa pekee kwa maisha ya jumuiya ya Kiislam na unampa kila mmoja nguvu mpya kwa ajili ya
maisha yake binafsi, familia na jamii. Kimsingi, ni muhimu kwa kila mmoja kutoa
ushuhuda wa ujumbe wa kiroho kwa maisha maadilifu zaidi kila mara, maisha
yanayoendana na mpango wa Muumba, katika ari ya kuwahudumia ndugu zake katika
amshikamano wa udugu, mara zote mkuu zaidi na wafuasi wa dini nyingine, na watu
wote wenye mapenzi mema katika nia ya kufanya kazi pamoja kwa faida ya wote.
2. Katika kipindi kigumu ambamo tunaishi, wafuasi wa dini mbalimbali, zaidi ya
yote wanalo jukumu la kufanya kazi kama wafuasi wa Mwenye Nguvu kwa ajili ya
amani inayoheshimu maoni binafsi ya mtu na ya kila jumuiya, kadhalika katika
uhuru wa kuabudu.Uhuru wa dini usiochujuliwa katika ufinyu wa uhuru wa kufanya
ibada tu, kimsingi ni moja ya vipengele muhimu vya uhuru wa dhamiri, ambao ni
haki ya kila mtu, na ambao ni jiwe la msingi la haki za
binadamu Ni
katika kutambua hilo, ndipo unapoweza kuendelezwa utamaduni wa amani na
mshikamano kati ya watu, na ambapo, kimsingi wote wanaweza kujituma katika
kujenga jamii yenye udugu zaidi, kwa kufanya kila kinachowezekana ndani ya uwezo
wao kukataa vurugu za aina yoyote ile, kwa kukemea na kupinga maelekeo ya
migogoro, yenye ushabiki wa kidini, kwani inajeruhi ndani ya mwanadamu sura ya
Mungu.
Sote tunajua kwamba migogoro na hasa ugaidi unaotendeka bila kuwa na macho na
unaosababisha majeruhi na wahanga wengi na hasa wasio na hatia, hauwezi kutatua
migogoro, na kwamba, zaidi unasababisha uchochezi mbaya wa chuki haribifu, kwa
hasara ya wanadamu na jamii.
3. Kama watu wa dini, ni jukumu la kila mmoja, awali ya yote , kuwa mlezi wa
amani, haki za binadamu, uhuru binafsi wa kila mmoja na pia maisha ya jamii bora
zaidi, kwani mwanadamu anawajibika kuwasaidia kaka na dada katika ubinadamu bila
baguzi wowote. Hakuna anayeweza kutengwa na jamii ya kitaifa kwa msingi wa
kabila lake,taifa na tabia zozote za kibinafsi. Sote pamoja, wa mapokeo tofauti
ya kidini, tunaitwa kueneza fundisho linalomheshimu kila mwanadamu, ujumbe wa
upendo kati ya watu na kati ya jamii.
Kimsingi, ni juu yetu, ndani ya mtazamo huu, kulea kizazi cha vijana,
watakaokuwa na majukumu katika ulimwengu wa kesho. Ni jukumu la kila mmoja,
kwanza familia, kisha watu wenye majukumu katika ulimwengu wa malezi na wote
wenye Mamlaka katika jamii na dini kuwajibika kuendeleza fundisho la haki, na
kutoa kwa kila mmoja malezi yanayolenga maeneo yaliyotajwa na hasa malezi ya
jamii, yanayomwita kila kijana kuwaheshimu wote wanaoishi nao na kuwajali kama
kaka na dada, ambao tumeitwa kuishi nao kila siku, siyo katika tofauti bali
katika heshima ya kindugu. Kwa hiyo, ni muhimu zaidi kukifundisha kizazi kipya
amali za kibinadamu, kimaadili, misingi jamii iliyo muhimu kwa maisha binafsi na
ya jamii.Ufidhuli wote wote ule, uwe ni wakati muafaka wa kuwakumbusha vijana
kuwa wanategemewa sana katika maisha ya jamii. Ni faida ya kila jamii na ulimwengu kwa pamoja ulio hatarini.
4. Katika mtazamo huu, hapana budi kuona kwamba ni muhimu maendelezo na
uimarishaji wa mazungumzano kati ya Wakristo na Waislamu, katika upeo wa malezi
na utamadunmi ili kuweka pamoja nguvu zote au huduma za mwanadamu na binadamu,
kusudi kizazi cha vijana kusijiundie makundi ya kitamaduni au ya kidini
yanayokinzana, bali uthabiti halisi wa kaka na dada katika ubinadamu.
Mazungumzano ni chombo kinachoweza kutusaidia kuondokana na mnyororo endelevu wa
migogoro na mivutano mingi inayozikumba jamii zetu, kusudi watu wote waweze
kuishi katika utulivu na amani, katika heshima kwa kila mmoja na maelewano
mazuri hata katika tofauti zinapojitokeza
Kwa sababu hiyo, katika matashi yangu haya natoa angalisho kwa wote, ili katika
mikutano na kushirikishana, Wakristo na Waislamu wafanye kazi pamoja kwa
kuheshimiana katika kujenga amani na kujenga ulimwengu pawe mahali pazuri pa
kuishi kwa watu wote. Huo utakuwa kwa vijana wa leo mfano wa kuiga na kufuata.
Kuanzia hapo vijana watajenga matumaini mapya katika maisha ya jamii na
watajitahidi zaidi katika kushiriki na kutimiza wajibu wao katika kuleta
mabadiliko. Malezi na mifano itakuwa kwa ajili yao pia chimbuko la matumaini kwa
baadaye.
5. Haya ndiyo matashi motomoto ninayoshiriki pamoja nanyi, kwamba Wakristo na
Waislamu zaidi na zaidi waendeleze mahusiano ya kirafiki na endelevu kwa
kushirikishana amali zao za pekee na kimsingi wajali thamani ya ushuhuda wa
imani ya waumini wao!
Wapendwa Waislamu, ninarudia tena matashi yangu mema kwenu yatokayo moyoni kwa
ajili ya sikukuu yenu, na ninamwomba Mungu wa amani na rehema awape ninyi nyote
afya njema, utulivu na fanaka.
Jean-Louis Card. Tauran
Rais
Pier Luigi Celata
Katibu