|
HALMASHAURI YA KIPAPA
KWA AJILI YA MAZUNGUMZANO NA DINI MBALIMBALI
Wakristo na Waislam:
Tuungane kushinda vurugu miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali
UJUMBE KWA AJILI YA MWISHO
WA RAMADHAN
‘Id al-Fitr 1431/2010
A.D.
Jijini Vatikani
Wapendwa Marafiki Waislam,
1. ‘ld Al-Fitr, inayohitimisha mwezi wa
Ramadhan, kwa mara nyingine, inatupa fursa nzuri, ili, kwa niaba
ya Halmashauri ya Kipapa kwa ajili ya Mazungumzano na Dini
mbalimbali, kuwaletea matashi ya moyoni kuwatakia utulivu na
furaha.
Mwezi huu wote mlijitoa kusali, kufunga,
kuwasaidia wahitaji, na kuimarisha mahusiano ya familia na
undugu. Mungu hataacha kuzibariki juhudi hizo!
2. Ninayo furaha kusema kwamba waumini wa dini
nyingine, kwa namna ya pekee Wakristo, wako karibu nanyi kiroho
katika siku hizi, kama inavyoshuhudiwa na mikutano mbalimbali ya
kirafiki, ambayo mara nyingi inawezesha mabadiliko asili ya
kidini. Ni furaha yangu kufikiri kwamba hata Ujumbe huu unaweza
kutoa mchango chanya kwa ajili ya tafakari zenu.
3. Mada iliyopendekezwa mwaka huu na
Halmashauri ya Kipapa: Wakristo na Waislam: Tuungane kushinda
vurugu miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali, kwa bahati
mbaya, ni suala lenye mbinyo, walau katika maeneo kadhaa
ulimwenguni. Kamati ya Pamoja kwa ajili ya mazungumzano
iliyoundwa na Halmashauri ya Kipapa na Kamati ya Kudumu kwa
ajili ya mazunguzano miongoni mwa dini zinazomwamini Mungu mmoja
ya al-Azhar zilichagua mada hii kwa ajili ya kujifunza,
kutafakari, na kubadilishana mawazo wakati wa mkutano wake wa
mwisho wa mwaka (Cairo, -23 - Februari 24, 2010). Mniruhusu
nishiriki nanyi hitimisho lilitolewa mwishoni mwa mkutano huu.
4. Kuna sababu nyingi zinazosababisha vurugu
miongoni mwa waumini wenye mapokeo mbalimbali ya dini, ikiwa ni
pamoja na: kupotosha lengo la dini kwa malengo ya kisiasa au
mengineyo; ubaguzi kwa misingi ya ukabila, utambulisho wadini;
migawanyiko na mivutano ya kijamii. Ujinga, umasikini, maendeleo
duni ni vyanzo vya moja kwa moja au visivyo wazi vya vurugu hata
ndani ya jumuiya za kidini. Ni vema serikali na viongozi wa dini
watoe mchango wao ili kuepusha mazingira mengi hivi kwa ajili ya
manufaa ya jamii nzima. Ni vema serikali zizingatie ubora wa
sheria katika kuhakikisha haki ya kweli ili kuwakomesha wazuaji
na waenezaji wa vurugu!
5. Yako pia mapendekezo muhimu yaliyotolewa na
matini iliyotajwa: kufungua mioyo yetu kwa ajili ya kusameheana
na kupatana, kwa ajili ya kukaa pamoja kwa amani kunakoleta
faida; kutambua kile tunachokuwa nacho kwa pamoja na kuheshimu
tofauti, kama msingi wa utamaduni wa mazungunzano; kutambua na
kujali heshima na haki za kila mwanadamu bila kuingiliwa na
upendeleo wowote unaohusiana na kabila au ushirikishwaji wa
kidini; lazima kuendeleza sheria za haki zinazowahakishia usawa
wa msingi kwa wote; kukumbuka umuhimu wa elimu kwa ajili ya
heshima, mazungumzano na udugu katika nyanja mbalimbali za
uelimishaji: nyumbani, shuleni, kanisani na misikitini. Kwa
namna hiyo tutaweza kuzishinda vurugu miongoni mwa wafuasi wa
dini mbalimbali na kukuza amani na mapatano miongoni mwa jumuiya
za dini mbalimbali. Mafundisho ya viongozi wa dini, kadhalika
vitabu vya shuleni vinavyoleta dini kwa namna iliyo halisi,
pamoja na ufundishaji kwa jumla, vina msukumo imara juu ya elimu
na malezi ya vizazi vipya.
6. Natumaini kwamba fikra hizi, hali kadhalika
na majibu ambayo yatayaibuliwa ndani ya jamii, na pamoja na
marafiki zenu Wakristo, zitachangia katika kuendeleza
mazungumzano, kukua katika heshima na utulivu, kwa ajili ya hayo
ninasihi Baraka za Mungu.
Jean-Louis Kardinali Tauran
Rais
Askofu Mkuu Pier Luigi Celata
Katibu
|