Wapendwa Marafiki Waislam,
1. Nina furaha ya pekee kuwapa matashi ya kirafiki na upendo kutoka kwa Halmashauri ya Kipapa kwa ajili ya Mazungumzano na Dini mbalimbali kwa nafasi ya furaha kwenu ya sikukuu ya ‘Id al-Fitri’, inayohitimisha safari yenu mliyoifanya wakati wa mwezi wa Ramadhan wa mfungo na sala.
Mchakato huu ni muda wa pekee kwa maisha ya jumuiya ya Kiislam na unampa kila mmoja nguvu mpya kwa ajili ya maisha yake binafsi, familia na jamii. Kimsingi, ni muhimu kwa kila mmoja kutoa ushuhuda wa ujumbe wa kiroho kwa maisha maadilifu zaidi kila mara, maisha yanayoendana na mpango wa Muumba, katika ari ya kuwahudumia ndugu zake katika amshikamano wa udugu, mara zote mkuu zaidi na wafuasi wa dini nyingine, na watu wote wenye mapenzi mema katika nia ya kufanya kazi pamoja kwa faida ya wote.
2. Katika kipindi kigumu ambamo tunaishi, wafuasi wa dini mbalimbali, zaidi ya yote wanalo jukumu la kufanya kazi kama wafuasi wa Mwenye Nguvu kwa ajili ya amani inayoheshimu maoni binafsi ya mtu na ya kila jumuiya, kadhalika katika uhuru wa kuabudu.Uhuru wa dini usiochujuliwa katika ufinyu wa uhuru wa kufanya ibada tu, kimsingi ni moja ya vipengele muhimu vya uhuru wa dhamiri, ambao ni haki ya kila mtu, na ambao ni jiwe la msingi la haki za binadamu Ni katika kutambua hilo, ndipo unapoweza kuendelezwa utamaduni wa amani na mshikamano kati ya watu, na ambapo, kimsingi wote wanaweza kujituma katika kujenga jamii yenye udugu zaidi, kwa kufanya kila kinachowezekana ndani ya uwezo wao kukataa vurugu za aina yoyote ile, kwa kukemea na kupinga maelekeo ya migogoro, yenye ushabiki wa kidini, kwani inajeruhi ndani ya mwanadamu sura ya Mungu.
Sote tunajua kwamba migogoro na hasa ugaidi unaotendeka bila kuwa na macho na unaosababisha majeruhi na wahanga wengi na hasa wasio na hatia, hauwezi kutatua migogoro, na kwamba, zaidi unasababisha uchochezi mbaya wa chuki haribifu, kwa hasara ya wanadamu na jamii.
3. Kama watu wa dini, ni jukumu la kila mmoja, awali ya yote , kuwa mlezi wa amani, haki za binadamu, uhuru binafsi wa kila mmoja na pia maisha ya jamii bora zaidi, kwani mwanadamu anawajibika kuwasaidia kaka na dada katika ubinadamu bila baguzi wowote. Hakuna anayeweza kutengwa na jamii ya kitaifa kwa msingi wa kabila lake,taifa na tabia zozote za kibinafsi. Sote pamoja, wa mapokeo tofauti ya kidini, tunaitwa kueneza fundisho linalomheshimu kila mwanadamu, ujumbe wa upendo kati ya watu na kati ya jamii.
Kimsingi, ni juu yetu, ndani ya mtazamo huu, kulea kizazi cha vijana, watakaokuwa na majukumu katika ulimwengu wa kesho. Ni jukumu la kila mmoja, kwanza familia, kisha watu wenye majukumu katika ulimwengu wa malezi na wote wenye Mamlaka katika jamii na dini kuwajibika kuendeleza fundisho la haki, na kutoa kwa kila mmoja malezi yanayolenga maeneo yaliyotajwa na hasa malezi ya jamii, yanayomwita kila kijana kuwaheshimu wote wanaoishi nao na kuwajali kama kaka na dada, ambao tumeitwa kuishi nao kila siku, siyo katika tofauti bali katika heshima ya kindugu. Kwa hiyo, ni muhimu zaidi kukifundisha kizazi kipya amali za kibinadamu, kimaadili, misingi jamii iliyo muhimu kwa maisha binafsi na ya jamii.Ufidhuli wote wote ule, uwe ni wakati muafaka wa kuwakumbusha vijana kuwa wanategemewa sana katika maisha ya jamii. Ni faida ya kila jamii na ulimwengu kwa pamoja ulio hatarini.
4. Katika mtazamo huu, hapana budi kuona kwamba ni muhimu maendelezo na uimarishaji wa mazungumzano kati ya Wakristo na Waislamu, katika upeo wa malezi na utamadunmi ili kuweka pamoja nguvu zote au huduma za mwanadamu na binadamu, kusudi kizazi cha vijana kusijiundie makundi ya kitamaduni au ya kidini yanayokinzana, bali uthabiti halisi wa kaka na dada katika ubinadamu. Mazungumzano ni chombo kinachoweza kutusaidia kuondokana na mnyororo endelevu wa migogoro na mivutano mingi inayozikumba jamii zetu, kusudi watu wote waweze kuishi katika utulivu na amani, katika heshima kwa kila mmoja na maelewano mazuri hata katika tofauti zinapojitokeza
Kwa sababu hiyo, katika matashi yangu haya natoa angalisho kwa wote, ili katika mikutano na kushirikishana, Wakristo na Waislamu wafanye kazi pamoja kwa kuheshimiana katika kujenga amani na kujenga ulimwengu pawe mahali pazuri pa kuishi kwa watu wote. Huo utakuwa kwa vijana wa leo mfano wa kuiga na kufuata. Kuanzia hapo vijana watajenga matumaini mapya katika maisha ya jamii na watajitahidi zaidi katika kushiriki na kutimiza wajibu wao katika kuleta mabadiliko. Malezi na mifano itakuwa kwa ajili yao pia chimbuko la matumaini kwa baadaye.
5. Haya ndiyo matashi motomoto ninayoshiriki pamoja nanyi, kwamba Wakristo na Waislamu zaidi na zaidi waendeleze mahusiano ya kirafiki na endelevu kwa kushirikishana amali zao za pekee na kimsingi wajali thamani ya ushuhuda wa imani ya waumini wao!
Wapendwa Waislamu, ninarudia tena matashi yangu mema kwenu yatokayo moyoni kwa ajili ya sikukuu yenu, na ninamwomba Mungu wa amani na rehema awape ninyi nyote afya njema, utulivu na fanaka.
Jean-Louis Card. Tauran
Rais
Pier Luigi Celata
Katibu