Index   Back Top Print

[ EN  - ES  - FR  - IT  - PL  - PT  - SW ]

PAPA FRANSISKO

Sala kwa Familia Takatifu *

 

 

Yesu, Maria na Yosefu,
ndani yenu tunatazama
mwangaza wa upendo wa kweli,
na tunawakimbilia kwa matumaini.

Familia takatifu ya Nazareti,
zifanye pia familia zetu
ziwe mahali pa ushirika na sala,
shule halisi ya Injili
na Makanisa madogo ya nyumbani.

Familia takatifu ya Nazareti,
isitokee tena kamwe kuwepo katika familia
ujeuri, ugumu wa moyo na matengano:
na kila aliyejeruhiwa au kukwazwa
apate mapema kufarijiwa na kuponywa.

Familia takatifu ya Nazareti,
Sinodi ya Maaskofu itakayoadhimishwa
iamshe tena moyoni mwa watu wote
ufahamu wa tabia takatifu ya familia isiyovunjika,
na uzuri wake katika mpango wa Mungu.

Yesu, Maria na Yosefu,
msikie na kusikiliza maombi yetu. Amina.

 

* Sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 29 Desemba, 2013

 


Copyright © Dicastero per la Comunicazione - Libreria Editrice Vaticana